USTAWI WA JAMII NCHINI INAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WATAALAMU WANAOPASWA KUHUDUMIA JAMII.
Imeelezwa kuwa
sekta ya Ustawi wa Jamii nchini inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa
wataalamu wanaopaswa kuhudumia jamii kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji, Kata na Halmashauri
ambapo kwa sasa mahitaji ni elfu 23 huku wataalam waliopo ikiwa ni 730
katika Halmashauri zote nchini.
Hayo yameelezwa na Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa wana Taaluma wa Ustawi wa Jamii nchini (TASWO) Bw Awadh
Mohamed katika mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa TASWO mkoa wa Manyara
uliofanyika wilayani Babati.
Amesema kuwa watoa
huduma za ustawi wa jamii ni wachache kwani wanaotakiwa ni elfu ishirini na
tatu lakini waliopo kwa sasa ni 730 katika Halmashauri zote nchini huku wakiwa hawakidhi
mahitaji ya jamii katika kutatua matatizo mbalimbali yakiwemo
ya familia, mtu mmoja mmoja na makundi yenye mgawanyiko.
Kwa upande wake
Mwenyekiti mpya wa TASWO Mkoa wa Manyara Ezekiel Assecheck amesema
kufunguliwa kwa tawi hilo mkoani humo kutasaidia kuandaa mipango mikakati ya
utoaji wa ushauri kwa Serikali na watoa huduma katika kuibua changamoto
mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.
Naye mjumbe wa bodi ya
TASWO Taifa, Songoro Msongo amewataka wanachama na viongozi waliochaguliwa kushirikiana,
kwani kila mtu ni wa muhimu katika kutoa mchango wake katika umoja
huo na kuweza kusonga mbele.
USTAWI WA JAMII NCHINI INAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WATAALAMU WANAOPASWA KUHUDUMIA JAMII.
Reviewed by safina radio
on
May 23, 2018
Rating:
No comments