MTOTO AUAWA KWA KUKATWA KICHWA NCHINI MALI.


Watu waliokuwa na silaha wamemuua kwa kumkata kichwa mtoto wa miaka mitano mwenye ulemavu wa ngozi albino nchini Mali.
Mtoto aliyefahamika kwa jina la Djeneba Diarra, aliibiwa na watu hao usiku wa manane wakati akiwa amelala nyumbani kwao pamoja na mama yake na dada yake, katika kijiji cha Fana nchini humo.
Mama mzazi mtoto huyo ameushuhudia mkasa huo akisema kuwa alijaribu kuwakimbiza watu hao waliomchukua mwanawe lakini baadae alirudi nyuma ili kumlinda mtoto wake mwingine ambaye pia ni albino.
Polisi nchini humo wamesema wanahofia kuwa mauaji hayo yalikuwa ni mauaji ya kishirikina na uchawi unaotegemea viungo vya albino ambapo Wengi wanauawa kwa kukatwa viungo vyao vya mwili,vinavyotumika katika uchawi unaoaminiwa kuleta utajiri na mafanikio katika maisha jambo ambalo sii kweli.
 Kwa kipindi cha nyuma mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yalikuwa ni tatizo kubwa katika nchi kadhaa za Kiafrika ikiwa ni pamoja na Malawi, Msumbiji,Tanzania na Zimbabwe pamoja na mataifa mengine ya Afrika Magharibi.

MTOTO AUAWA KWA KUKATWA KICHWA NCHINI MALI. MTOTO AUAWA KWA KUKATWA KICHWA NCHINI MALI. Reviewed by safina radio on May 16, 2018 Rating: 5

No comments