FATOU BENSOUDA AKAMILISHA ZIARA YAKE DRC


Mwendesha mashtaka wa mahakama ya Kimataifa ya ICC Fatou Bensouda amekamilisha ziara yake nchini DRC ambako amekutana na watu mbali mbali akiwemo rais Joseph Kabila.

Image result for PICHA YA FATOU BENSOUDA MWENDESHA MASHTAKA ICC
FATOU BANSOUDA.
 Fatou Bensouda, alikutana na Joseph Kabila huko Kinshasa, ambapo  walijadili vurugu katika DRC, hali ya mahakama ya kitaifa na ushirikiano kati ya Ofisi ya ICC na DRC.
Bensouda pia  alikutana na  bazara la maaskofu, upinzani, wanasheria na mashirika ya kiraia na  kuulizia hali ya haki za binadamu.
Kwa mujibu wa Fatou Bensouda, serikali ina jukumu la msingi la kuanzisha kesi za kisheria dhidi ya wahalifu wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC kwa lengo la kukomesha kutokujali na kurejesha hali ya haki na amani nchini.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Kidemocratia ya Congo, Flory Kabange Numbi, alimhakikishia Mwendesha Mashitaka wa ICC uamuzi wa mamlaka za Kinshasa kuchunguza kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu na kufungua mashitaki dhidi ya wahalifu hao.
Hata hivyo Mnamo Machi 2016, afisa mkuu wa ICC Margot Tedesco, alisema kuwa Mahakama ya ICC tayari imepokea taarifa kuhusu mauaji huko Beni, Kivu kaskazini .


FATOU BENSOUDA AKAMILISHA ZIARA YAKE DRC FATOU BENSOUDA AKAMILISHA ZIARA YAKE DRC Reviewed by safina radio on May 04, 2018 Rating: 5

No comments