RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUITUNZA AMANI.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John
Magufuli amewataka watanzania kuendelea kuitunza na kuilinda amani iliyoko hapa
nchini kwani palipo na amani ndipo penye maendeleo.
RAIS MAGUFULI |
Mh Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza
na wananchi wa eneo la Ilula mkoani Iringa akiwa njiani kuelekea mkoani
Morogoro,ambapo amesema kuwa Tanzania imejengwa katika misingi ya upendo na
amani hivyo ni vyema Watanzania wakaienzi misingi hiyo bila kujali makabila
yao.
Ameongeza kuwa kukiwa na amani wawekezaji kutoka nje
ya nchi watakuja kuwekeza hapa nchini na uchumi wa Tanzania utakuwa kwa
kasi,huku akiwataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaotaka kuleta vurugu hapa
nchini kwa kurubuniwa kwa njia mbalimbali na watu wasioitakia mema Tanzania.
Aidha akiwa katika eneo la Ruaha Mbuyuni rais
Magufuli aliweza kukabidhi kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi
wa hospitali ya
Ruaha,ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea
kuboresha sekta ya afya kwa kutenga bajeti zaidi katika wizara ya afya.
Hata hivyo rais Mgufuli ameondoka mkoani Iringa,na
kwa sasa yupo mkoani Morogoro ambapo atazindua ujenzi wa barabara ya Kidatu
hadi Ifakara.
RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUITUNZA AMANI.
Reviewed by safina radio
on
May 04, 2018
Rating:
No comments