TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAENDELEA.


 Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Bw Raymond Mushi amesema kuwa lipo tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na hasa miongoni mwa vijana jambo ambalo linazidi kukua kila mwaka kutokana na vijana wengi kuwa wasomi na kubagua kazi.

Image result for PICHA YA MKUU WA WILAYA YA BABATI RAYMOND MUSHI
MKUU WA WILAYA YA BABATI RAYMOND MUSHI.
 Bw Mushi ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari wilayani humo namna serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga kukuza uchumi wake kwa njia ya viwanda ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Amesema ajira zitaongezeka endapo uchumi utakuwa,yaani shughuli za uzalishaji mali na utoaji wa huduma na shughuli zote hizo zinategemea kuongezeka kwa Uwekezaji kwani bila uwekezaji kuongezeka hakutokuwa na ongezeko la ajira kwa Vijana.

Mkuu huyo ameongeza kuwa serikali iliona tatizo la ajira kuwa kubwa ndio maana imejipanga kuondoa tatizo la ajira kwa kutekeleza ilani ambazo zinalenga kuwezesha nchi ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati inayoongozwa na viwanda.

Kwa upande wake mmoja wa mmiliki wa kiwanda cha Mati Super Brand Bw Gasper Mlay amesema kuwa ili Tanzania iweze kuendelea inawapasa kulipa kodi ili kuweza kujenga Barabara bora, kununua madawa hospitalini  na maji safi,kwani hivyo vyote vikikosekana hata mfanyabiashara hatoweza kufanya biashara vizuri.

TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAENDELEA. TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAENDELEA. Reviewed by safina radio on May 04, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.