MALORI MAWILI YAKAMATWA LONGIDO
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa
Arusha imekamata malori mawili katika eneo la Longido yaliyokuwa yakisafirisha
bidhaa za sukari pamoja na mafuta ya kupikia kinyume na sheria zenye kugharimu
fedha zaidi ya shilingi milioni 20.
BW KICHERE. |
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa
habari Kamishna Mkuu wa Mapato Tanzania Charles Kichere amesema kuwa usiku wa
kuamkia tarehe 11 katika maeneo ya Longido gari lenye namba za uasjili T 985
AJP na T 840 ABFyalikamatwa yakiwa yamepakia bidhaa za magendo.
Amesema kuwa Katika uchunguzi
uliofanyika ulibaini kuwepo kwa bidhaa mbalimbali ambapo katika lori la kwanza
kulikuwa na mifuko 193 ya sukari yenye ujazo wa kilo 50 kila mmoja huku katika
lori la pili kukiwa na mifuko 169 ya sukari yenye ujazo wa kilo 50 kila mmoja,
maboksi 40 ya mafuta ya kupikia aina ya Karibu yaliyofungwa kwa ujazo tofauti.
Amesema kuwa katika boksi hizo
kulikuwepo na kopo 24 zenye ujazo wa nusu lita kila moja,makopo 12 yenye ujazo
wa kilo mbili kila moja, makopo 12 yenye ujazo wa kilo moja kila moja,boksi 3
za mafuta ya kupikia aina ya Daria yenye makopo 12 kwa ujazo wa kilo moja kwa kila
moja.
Aidha kamishna huyo amesema kuwa jumla
ya thamani ya bidhaa hizo ni zaida ya shilingi milioni 20 ambapo kodi ya bidhaa
hizo ni zaidi ya shilingi milioni 28 huku adhabu na faini ya bidhaa hizo ikiwa
ni zaidi ya shilingi milioni 10 na kufanya jumla kuu ya mapato yanayotakiwa
kulipwa serikalini kufikia zaidi ya shilingi milioni 39.
MALORI MAWILI YAKAMATWA LONGIDO
Reviewed by safina radio
on
May 16, 2018
Rating:
No comments