MASHAMBULIZI YATISHIA SEKTA YA UTALII AFRIKA YA KUSINI


Wabunge wa Afrika Kusini wameonya kuwa mashambulizi dhidi ya watalii nchini humo yanatishia sekta ya utalii, ambayo imekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi katika nchi hiyo.

Image result for PICHA YA BUNGE LA AFRIKA YA KUSINI


Kauli hiyo imetolewa baada ya watalii watatu wa Ujerumani kuporwa mali zao Jumapili na watu wanne katika eneo la Ballito, karibu na mji wa Durban, mashariki mwa Afrika Kusini.

Watalii hao wamekumbwa na shambulizi hilo wakati wakielekea katika uwanja wa ndege wa King Shaka, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Kaimu mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji na utalii ya bunge la Afrika Kusini Bi Lusizo Makhubele-Mashele amesisitiza kuwa tishio lolote la kiusalama kwenye sekta hiyo, litaleta athari mbaya.

 Bi Lusizo ametoa wito kwa idara za utekelezaji wa sheria ziwafikishe wahalifu hao mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.


MASHAMBULIZI YATISHIA SEKTA YA UTALII AFRIKA YA KUSINI MASHAMBULIZI YATISHIA SEKTA YA UTALII AFRIKA YA KUSINI Reviewed by safina radio on May 15, 2018 Rating: 5

No comments