UBAELGIJI YAELEZA SABABU YAKUMUITA BALOZI WAKE KUTOKA CONGO DRC.


Serikali ya Ubelgiji imeeleza sababu za kumuita balozi wake nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya congo tangu mwezi January mwaka huu, baada ya nchi hiyo kuwa na mahusiano mabaya ya kidiplomasia na serikali ya kinshasa.
Image result for PICHA YA BENDERA YA UBELGIJI
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Didier Reinders alithibitisha Jumatatu wiki hii uamuzi wa Brussels wa kumrejesha nyumbani balozi wake aliyekuwa jijini Kinshasa Bertrand de Crombrugghe, akieleza kuwa mazingira ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili hayakuwa mazuri huku akiishutumu serikali ya DRC kushindwa kuonyesha ushirikiano katika masuala mengi ikiwemo ya kijeshi lakini pia kisiasa.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Ubelgiji hali kadhalika vyanzo vya kidiplomasia vimeripoti kuwa kulikuwa na uvunjaji wa uaminifu kati ya nchi hiyo ambayo iliitawala kikoloni DRC na serikali ya Kinshasa baada ya kutangazwa uamuzi wa kufungwa kwa ubalozi mdogo wa shengen, hatua ambayo ilionekana kuchochea uhasama zaidi.
Balozi Bertrand de Crombrugghe kwa upande wake amesema kuwa Wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji ilishangazwa na hatua ya Kinshasa baada ya yeye kupokea barua ya kumtaka aondoke nchini humo.
Ubelgiji imekuwa ikiitaka serikali ya Kinshasa kuboresha mazingira ya kisiasa na kuhakikisha makubaliano yaliyosainiwa chini ya upatanisho wa kanisa Katolijki CENCO yanatekelezwa, na uchaguzi unafanyika chini ya misingi ya kidemokrasia nchini humo.


UBAELGIJI YAELEZA SABABU YAKUMUITA BALOZI WAKE KUTOKA CONGO DRC. UBAELGIJI YAELEZA SABABU YAKUMUITA BALOZI WAKE KUTOKA CONGO DRC. Reviewed by safina radio on May 01, 2018 Rating: 5

No comments