RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli leo amefanya ziara ya
kushtukiza kwenye bandari ya Dar-es-salaam kukagua matenki ya mafuta ya kupikia
kufuatia kuwepo kwa taarifa ya mafuta kuzuiliwa bandarini wakati wananchi
wanahofia kupanda kwa bei ya mafuta hayo muda sii mrefu.
Mara baada ya Rais Magufuli
kuwasili bandarini,kwanza alipokea maelezo ya Wataalam mbalimbali wanaohusika
kulifatilia sakata hilo ambapo mmoja wa maafisa wa TRA ambaye alimwambia Rais
kuwa kwenye taarifa ya mafuta iliyotolewa kuna udanganyifu.
Aidha Rais Magufuli amebaini kuwa baadhi ya makontena yaliyodaiwa kuwa
na mafuta ghafi ya kupikia yalikuwa na mafuta masafi ambapo amesema kuwa baadhi
ya wafanyabiashara wanatumia nafasi zao kuwalaghai wananchi na kutaka mafuta
ghafi kutozwa bei ya juu ili kulinda viwanda vya ndani.
Hata hivyo amemtaka
mkemia mkuu wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na maadili na
kuweka maslahi ya taifa mbele.
Wakati huohuo Rais
Magufuli amempandisha cheo kamishina wa TRA bandari ya Dar es salaam Bw. Ben
Usaje kuwa kamishina kamili wa TRA bandarini hapo kufuatia kusimamia vyema
uchunguzi alioagiza ufanyike bandarini hapo.
RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI.
Reviewed by safina radio
on
May 15, 2018
Rating:
No comments