SERIKALI YAZIAGIZA HALMASHAURI KUTOA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA,NA WENYE ULEMAVU.
Serikali imeziagiza
Halmashauri zote Nchini kutoa fedha za mikopo ya asilimia kumi ya mapato yao
kwa wanawake,vijana,na watu wenye ulemavu bila kuwatoza riba yoyote.
MH. JAFFO. |
Agizo hilo
limetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mh. Selemani Jaffo alipokuwa akizungumza na
wafanyabiashara wa soko la Magomeni lengo likiwa ni kuzungumzia hatma ya
wafanyabiashara wa soko hilo katika siku za usoni.
Takribani shilingi
bilioni 9 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa soko la Magomeni ikiwa ni
mwendelezo wa serikali wa kuboresha masoko na vituo vya mbasi nchini ili
zifanyekazi kwa ufanisi.
SERIKALI YAZIAGIZA HALMASHAURI KUTOA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA,NA WENYE ULEMAVU.
Reviewed by safina radio
on
May 11, 2018
Rating:
No comments