SERIKALI IMESEMA INATAMBUA MCHANGO WA MWANA,KE.


Serikali imesema kuwa inatambua mchango wa mwanamke kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla na kwa sababu hiyo ndio maana serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili mikopo ya wanawake na vijana.

Hayo yamesemwa mapema leo bungeni jijini Dodoma na naibu waziri wa fedha na mipango Mh. Dk. Ashantu Kijaji wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Mh.  Bupe Mwakang’ata aliyetaka kujua ni lini serikali itawawezesha wanawake kibenki hususani wanaoishi katika mikoa ya pembezoni.
    
Image result for PICHA YA ASHATU KIJAJI
DK. KIJAJI.
                                          
Hata hivyo bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti za wizara mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.



SERIKALI IMESEMA INATAMBUA MCHANGO WA MWANA,KE. SERIKALI IMESEMA INATAMBUA MCHANGO WA MWANA,KE. Reviewed by safina radio on May 16, 2018 Rating: 5

No comments