RAIS TRUMP KUPUNGUZA IDADI YA WANAJESHI KOREA KUSINI


Rais wa Marekani Donald Trump ameigaiza wizara ya ulinzi nchini humo kujitayarisha kupunguza idadi ya wanajeshi wa Marekani walioko nchini Korea Kusini.
Image result for PICHA YA TRUMP
RAIS TRUMP WA MAREKANI
Gazeti la Marekani la New York Times limeripoti kuwa kupunguzwa kwa idadi ya wanajeshi hao hakulengi kuwa mojawapo ya vigezo kuelekea mkutano wa kilele kati ya Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
 Kutokana na makubaliano ya amani kati ya Korea Kusini na Kaskazini huenda yakapunguza haja ya kuwepo wanajeshi zaidi ya elfu ishirini na tatu  wa Marekani katika rasi ya Korea.
Mahusiano kati ya Korea mbili yameimarika hasa baada ya Korea Kaskazini kutangaza mwezi uliopita kuwa itaachana na mpango wake wa kinyuklia na viongozi wa nchi hizo mbili kukutana kwa mkutano wa kihistoria.


RAIS TRUMP KUPUNGUZA IDADI YA WANAJESHI KOREA KUSINI RAIS TRUMP KUPUNGUZA IDADI YA WANAJESHI KOREA KUSINI Reviewed by safina radio on May 04, 2018 Rating: 5

No comments