ZAIDI YA VYUO VIKUU 20 AFRIKA ZATARAJIA KUINGIZA MITAALA YA KILIMO HIFADHI.
ARUSHA.
Zaidi ya vyuo vikuu vya kilimo 20 barani Afrika vinatarajia kuingiza
mitaala ya kilimo hifadhi katika vyuo vyao ili kuwawezesha maafisa ugani
wanaohitimu katika vyuo hivyo kupata elimu ya kilimo hicho na baadaye
kuwafikishia wakulima ambao bado hawajafikiwa na elimu ya kilimo hifadhi.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika
la kilimo hifadhi barani Afrika Bw Saidi Mkomwa alipokuwa akizungumza
katika semina ya wadau wa matrekta ya kuwaonesha namna ya kutumia trekta katika
kilimo hifadhi iliyofanyika jijini Arusha.
Bw Mkomwa amesema kuwa
katika uhamasishaji wa wakulima juu ya kulima kilimo hifadhi shirika hilo
tayari limewakutanisha watoa elimu wa vyuo vikuu vya kilimo ili
kuangalia namna ya kuingiza mitaala hiyo ili kilimo hifadhi kifundishwe
katika vyuo hivyo kwa lengo la kuwezesha wahitimu kupata utaalamu wa
kuwaelekeza wakulima huko waendako.
Ameongeza kuwa hadi sasa Tanzania inalima hekta
elfu 30 za kilimo hifadhi huku kiwango hicho kikiwa ni cha chini kuliko nchi za
bara la Afrika ambapo idadi hiyo inatokana na ukosefu wa elimu kwa wakulima juu
ya kulima kilimo hifadhi ambacho kwa sasa ndicho kilimo
chenye tija kwani uzalishaji wake ni mkubwa zaidi kuliko kilimo cha mazoea.
Hata hivyo amesema kuwa wanaendelea kushirikiana na shirika
la kilimo hifadhi tanzania ili kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na
kuwasaidia wadau kuachana na kilimo cha kawaida na kulima kilimo hifadhi .
ZAIDI YA VYUO VIKUU 20 AFRIKA ZATARAJIA KUINGIZA MITAALA YA KILIMO HIFADHI.
Reviewed by safina radio
on
May 23, 2018
Rating:
No comments