VIWANDA VYA SARUJI VINACHANGAMOTO YA KUTOKUWA NA MIUNDOMBINU YA KUDHIBITI VUMBI KATIKA VIWANDA VYA SARUJI NA CHOKAA.


Imeelezwa kuwa viwanda vya saruji na chokaa vilivyoko mkoani Tanga vinakabiliwa na changamoto ya  kutokuwa na miundombinu thabiti ya kudhibiti vumbi kutoka viwandani hali inayochangia uchafuzi wa mazingira na migogoro kwa wananchi.

Image result for kiwanda cha saruji tanga

Hayo yamesemwa na katibu tawala wa mkoa huo Bi Anuciata Lyimo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na jinsi ambavyo wamekuwa wakikabiliana na utunzaji wa mazingira mkoani humo.

Amesema kuwa pamoja na kuendelea kutoa  elimu ya utunzaji mazingira lakini bado viwanda vya saruji na chokaa vinakabiliwa na changamoto ya kudhibiti vumbi kutoka viwandani hali inayochangia uchafuzi wa mazingira.

Aidha ameongeza kuwa katika sekta ya mazingira  bado baadhi ya viwanda ikiwemo cha Korona cha kuchakata mkonge hutiririsha maji taka kwenye vyanzo vya maji hivyo kuhatarisha afya za watumiaji wengine wa maji.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwa mafanikio mbali mbali yamepatikana katika utekelezaji wa sheria ya mazingira  bado wanaendelea na Ukaguzi wa Usafi wa Mazingira kwa ngazi ya kata na Vijiji na  kufuata Usimamizi wa agizo la kufanya usafi wa mazingira kwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kudhibiti changamoto hizo.

VIWANDA VYA SARUJI VINACHANGAMOTO YA KUTOKUWA NA MIUNDOMBINU YA KUDHIBITI VUMBI KATIKA VIWANDA VYA SARUJI NA CHOKAA. VIWANDA VYA SARUJI VINACHANGAMOTO YA KUTOKUWA NA MIUNDOMBINU YA KUDHIBITI VUMBI KATIKA VIWANDA VYA SARUJI NA CHOKAA. Reviewed by safina radio on May 02, 2018 Rating: 5

No comments