SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI VIJANA NCHINI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi
Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Anthon Mavunde amesema kuwa serikali inaendelea
kuweka mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana ili kuhakikisha
wanapata ajira.
MH. ANTHON MAVUNDE |
Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano
Kivuli la Vijana wa Umoja wa Mataifa jijini Dodoma lililowakutanisha vijana
kutoka nchi mbali mbali kujadili changamoto zinazowakabili vijana Duniani ili
kuzipatia ufumbuzi.
Aidha, amesema kuwa serikali ya Tanzania
imedhamiria kumkwamua kijana wa
kitanzania hasa katika kumpatia ujuzi stahiki ambapo ofisi ya Waziri Mkuu
inaendesha mafunzo kupitia Programu ya
Ukuzaji Ujuzi ya Miaka Mitano.
Mh. Mavunde amebainisha kuwa Mpango huo wa Programu
ya Miaka mitano inalenga kuwafikia vijana Milioni nne na Laki nne kwa ajili ya
kulenga vijana wote wawe na ujuzi stahiki katika dunia ya leo.
Hata hivyo Naibu Waziri Mavunde amewataka vijana
kutumia mitandao ya kijamii kutafuta fursa za kimaendeleo.
SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI VIJANA NCHINI
Reviewed by safina radio
on
May 01, 2018
Rating:
No comments