ZAIDI YA WATU 60 WAUAWA KATIKA JIMBO LA ADAMAWA, NIGERIA.


Watu zaidi ya 60 wameuawa katika jimbo la Adamawa, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu yaliyolenga msikiti na soko.
Image result for MAUAJI YA WATU 60 KATIKA JIMBO LA ADAMAWA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA
Licha ya kuwa hakuna mtu au kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi hayo, mji wa Mubi katika jimbo la Adamawa kaskazini mashariki mwa Nigeria, umekua ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram,ambapo mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita, watu 50 waliuawa katika mashambulizi ya awali.
Hata hivyo maafisa wa usalama wanasema mashambulizi hayo ya kujitoa mhanga, yalitekelezwa na wavulana wadogo waliotumwa na kundi la Boko Haram.
Waathirika wote walipelekwa katika hospitali nne tofauti katika mji wa Mubi na maeneo jirani.
Aidha mauaji hayo yametokea siku moja tu baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kukutana na kufanya mazungumzo katika ikulu ya White House na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na kuahidi kuisaidia nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika kupambana na makundi ya wabeba silaha.

ZAIDI YA WATU 60 WAUAWA KATIKA JIMBO LA ADAMAWA, NIGERIA. ZAIDI YA WATU 60 WAUAWA KATIKA JIMBO LA ADAMAWA, NIGERIA. Reviewed by safina radio on May 02, 2018 Rating: 5

No comments