TRUMP KUKUTANA NA KIM JONG UN JUN 12 NCHINI SINGAPORE.
Rais
wa Marekani, Donald Trump amesema atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim
Jong Un Juni 12 nchini Singapore.
RAIS TRUMP. |
Mkutano
huo wa kilele utakuwa wa kihistoria na wa aina yake kati ya viongozi hao wawili
ambapo Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba watajitahidi
kuufanya mkutano huo uwe wa muhimu kwa ajili ya amani ya dunia.
Viongozi
hao wawili wanatarajia kujadiliana kuhusu maendeleo ya silaha za nyuklia za
Korea Kaskazini pamoja na majaribio yake ya makombora ambayo yamesababisha
mvutano wa muda mrefu kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN |
Tangazo
hilo la Trump limetolewa muda mchache baada ya raia watatu wa Marekani
waliokuwa wamefungwa gerezani Korea Kaskazini kuwasili Marekani, baada ya
kuachiwa huru na utawala wa Kim.
Trump
amesema atafurahi kama watafanikiwa kuhakikisha hakuna kabisa silaha za nyuklia
katika Rasi ya Korea.
TRUMP KUKUTANA NA KIM JONG UN JUN 12 NCHINI SINGAPORE.
Reviewed by safina radio
on
May 11, 2018
Rating:
No comments