WATU ZAIDI YA 40 WAFARIKI NCHINI KENYA
Zaidi ya watu 40 wamefariki na maelfu ya wengine kuachwa bila makazi
wakati bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano
usiku.

Shirika la kupambana
na majanga nchini Kenya linasema kuwa hadi sasa watu wengi hawajulikani waliko ambapo
Maafisa wa uokozi kutoka mashirika tofauti nchini humo wanaendelea na jitihada
za kutafuta miili ya watu waliokufa kutokana na mkasa huo.
Eneo hilo la Solai
katika kaunti ya Nakuru nchini Kenya, lina mabwawa saba yanayotumika katika
kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya
Fred Matiang'i amesema serikali imeanzisha uchunguzi kubaini uthabiti wa
mabwawa mengine sita yaliosalia.
Mapema leo Ijumaa kulikuwa na hisia ya wasiwasi baada ya taarifa kusambaa
katika mitandao ya kijamii kwamba bwawa la pili limepasuka katika eneo hilo.
WATU ZAIDI YA 40 WAFARIKI NCHINI KENYA
Reviewed by safina radio
on
May 11, 2018
Rating:
No comments