MWEZI JANUARI BUNGE LA EU LILIOMBA ICC NA UN KUCHUNGUZA VISA VYA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU.
Kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC yupo
jijini Kinshasa nchini DRC, baada ya kupokea maombi ya ofisi yake kuchunguza
visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Bensuda anakutana na viongozi wa serikali na maafisa wa
Mahakama, na anatarajiwa kuzungumzia ziara yake hapo kesho.
Mwezi Januari Bunge la Umoja wa Ulaya liliomba ICC na Umoja wa
Mataifa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyokuwa
vimeshuhudiwa katika jimbo la Kasai.
Wakati huo huo polisi nchini DRC imewaachilia huru wanaharakati
wa Lucha waliokuwa wamekamatwa walipokuwa wanapanga kuwa na mkutano wa hadhara
mjini Goma.
Wanaharakati 27 walikamatwa akiwemo kiongozi wao Rebecca Kavugho
ambaye alipata tuzo kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kama mwanamke
shupavu.
Polisi wamesema wamewaachia huru wanahaharkati hao baada ya
kubainika kuwa hawakuwa na kosa lolote.
MWEZI JANUARI BUNGE LA EU LILIOMBA ICC NA UN KUCHUNGUZA VISA VYA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU.
Reviewed by safina radio
on
May 02, 2018
Rating:
No comments