WAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI UNAOTOLEWA NA WATAALAM
Wakulima hapa
nchini wametakiwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo ili waweze
kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayoshambulia
mazao yao.
Ushauri huo umetolewa
na afisa ugani wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania mkoa wa Manyara Bw
Donald Laizer wakati akizungumza na Redio Safina kuhusu magonjwa mbalimbali yanayoshambulia
zao la mahindi na maharage mkoani humo.
Amesema kuwa
kutokana na wakulima wengi kutofuata ushauri unaotolewa na wataalamu wameshindwa
kujua namna ya kupambana na magonjwa hayo haswa ugonjwa wa kutu unaosababisha
mahindi na maharage kunyauka.
Kwa upande wa
wakulima wa kijiji cha Gedemara kata ya Galapo mkoani Manyara wamesema kuwa
katika kilimo chao wanakabiliwa na changamoto kubwa ya mazao yao kunyakua pamoja
na mabadiliko ya hali ya hewa.
WAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI UNAOTOLEWA NA WATAALAM
Reviewed by safina radio
on
May 11, 2018
Rating:
No comments