CHANJO YA KICHAA CHA MBWA YAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO
kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro limezindua kampeni ya chanjo
ya kichaa cha mbwa na paka ambapo mbwa elfu thelathini na mbili watapatiwa
chanjo hiyo.
Akizungumzia kampeni hiyo katika kata ya Kindi
wilaya ya Moshi Afisa Mwandamizi kutoka FAO Farus Rafina amesema kuwa wamiliki
wa Mbwa pia watapewa elimu ya kukabiliana na ugonjwa huo wa kichaa cha Mbwa.
Akitoa taarifa ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa
Mkoa wa Kilimanjaro Daktari wa Mifugo mkoani humo Dk. Emanuel Lema amesema kuwa
kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 mbwa wapatao 570 wamebainika kuwa na kichaa cha
mbwa huku watu zaidi ya elfu nane waking’atwa na mbwa.
Akishuhudia Uzinduzi wa Chanjo hiyo Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Anna Nghwira amesema kuwa uzuiaji na udhibiti wa mfumo wa chanjo
utazuia ugonjwa huo kwa binadamu.
CHANJO YA KICHAA CHA MBWA YAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO.
Reviewed by safina radio
on
May 04, 2018
Rating:
No comments