RAIS MAGUFULI ATAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUANZISHA MIFUKO YA DAWA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John
Pombe Magufuli amezitaka Halmashauri zote Nchini kuanzisha mifuko ya dawa ili kurahisisha manunuzi
ya dawa, Vitendea Kazi mbali mbali pamoja na vifaa vingine vya matibabu.
Dk. Magufuli ametoa agizo hilo leo Mkoani Iringa
wakati wa Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo,
ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi
Bilioni 4.2 ambayo itakuwa na X-rays, pamoja na chumba cha upasuaji.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Bima ya
Afya ambayo itawarahisishia kupata
huduma za Afya kwa urahisi pamoja na kupunguza gharama za upatikanaji wa
matibabu,ambapo pia serikali imetenga jumla
ya shilingi bilioni 50 kwa ajili kununuliwa vifaa vya Hospitali kote nchini.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais tawala
za mikoa na serikali za mitaa Mh Suleman Jaffo amesema kuwa kukamilika kwa
hospitali hiyo kutaongeza idadi ya hospitali za wilaya hapa nchini kufikia 77.
Amesema kuwa kwa sasa serikali inaendelea na ujenzi
wa hospitali za wilaya nne hapa nchini ikiwemo wilaya za Buchosa,Siha na Kilolo huku
ikiendelea na ujenzi wa vituo vya afya 208.
RAIS MAGUFULI ATAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUANZISHA MIFUKO YA DAWA.
Reviewed by safina radio
on
May 02, 2018
Rating:
No comments