RAIS KENYATA AIDHINISHA SHERIA ZA UHALIFU WA KOMPYUTA.
RAIS KENYATA |
Sheria hiyo inatoa
adhabu ya faini ya Shilingi milioni 5 ya Kenya sawa dola elfu hamsini za
Marekani au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana
na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.
Pia mswada huo wa
sheria unaeleza kuwa mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo
zinaweza kuzua taharuki au vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.
Baadhi ya wadau
wanasema kuwa sheria hiyo inatarajiwa kuathiri utendaji kazi wa wanahabari,
vyombo vya habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii, wanavitalu na watu wengine
wanaotumia kompyuta na mitandao.
Kiongozi wa zamani wa
Chama cha Wanasheria Kenya Apollo Mboya amenukuliwa na vyombo vya habari
akisema kifungu hicho kinaweza kuwapa watawala,uhuru wa kukandamiza vyombo vya
habari.
RAIS KENYATA AIDHINISHA SHERIA ZA UHALIFU WA KOMPYUTA.
Reviewed by safina radio
on
May 16, 2018
Rating:
No comments