SERIAKALI KUENDELEA KUBORESHA VITUO VYA AFYA HAPA NCHINI.
Serikali imesema kuwa inaendelea kuboresha na
kumalizia ujenzi wa vituo vya afya 208 kote nchini ili kuboresha utoaji wa
huduma za afya karibu na wananchi kwa lengo la kuwapunguzia changamoto za
kufuata huduma hizo umbali mrefu.
MH. KAKUNDA |
Hayo yamesemwa leo bungeni jijini
Dodoma na naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa
Tamisemi Mh. Joseph Kakunda wakati akijibu swali la mbunge wa Rungwe Mh Saul
Henry Amon aliyetaka kujua ni lini serikali itamalizia vituo vya afya ambavyo
bado ujenzi wake haujakamilika.
Mh Kakunda amesema kuwa katika
halmashauri ya wilaya ya Rungwe serikali imepeleka shilingi bilioni moja ambapo
mwezi septemba mwaka 2017 serikali ilipeleka shilingi milioni mia tano kwenye
kituo cha afya cha Ikuti kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje
OPD,chumba cha upasuaji,wodi ya watoto na wodi ya mama wajawazito.
Wakati huo huo serikali imesema kuwa
katika mwaka wa fedha 2018/2019 imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.2
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini katika halmashauri ya
wilaya ya Monduli.
MH. AWESO |
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa maji
na umwagiliaji Mh. Juma Aweso wakati akijibu
swali la mbunge wa Monduli Mh. Julius Kalanga laizer aliyetaka kujua ni lini
serikali itatimiza ahadi ya rais ya ukarabati ya mabwawa matatu wilayani
Monduli.
SERIAKALI KUENDELEA KUBORESHA VITUO VYA AFYA HAPA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
May 15, 2018
Rating:
No comments