WAZIRI JAFFO AKATAA GHARAMA ZA UJENZI WA BWENI.


Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa  Tamisemi Mh. Selemani Jaffo amesema hajaridhishwa na mradi wa ujenzi wa bweni la shule ya Endasak wilayani Hanang mkoani Manyara kutokana na matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni  170.6

Waziri Jaffo ameeleza kutoridhishwa kwake na mradi huo kwani halmashauri nyingine zinatumia fedha kiasi cha shilingi milioni mia moja na hamsini kujenga mabweni mawili.
        Image result for PICHA YA WAZIRI JAFFO                              

Hata hivyo waziri Jaffo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Endasak amesema kuwa serikali ina mpango wa kuongeza shule za sekondari wilayani Hanang.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi mradi huo Mwalimu Gisela Msofe amesema kuwa mradi huo wa bweni lenye vyumba ishirini litakalo chukua wanafunzi 80  umefadhiliwa na taasisi ya elimu TEA.



WAZIRI JAFFO AKATAA GHARAMA ZA UJENZI WA BWENI. WAZIRI JAFFO AKATAA GHARAMA ZA UJENZI WA BWENI. Reviewed by safina radio on May 16, 2018 Rating: 5

No comments