AL SHABAB YAWASHAMBULIA AMISOM


Kundi la Al Shabab nchini Somalia limetekeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) na jeshi la Somalia katika mkoa wa Shabelle, kusini mwa Mogadishu.
Msemaji wa Al Shabab alisema wapiganaji wake 14 waliuawa huku wanajeshi 59 wa AU wakiuawa.

Kundi hilo linasema kuwa lilitekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya kambi za kikosi hicho kinachosimamia amani na usalama nchini Somalia.
Kundi la Al Shabab linasema liliwaua askari 59 wa Amisom, wengi wao ni kutoka Uganda, na lilipoteza wapiganaji wake 14 katika vita hivyo huku jeshi la Uganda likisema kuwa wamepoteza  askari wake wanne na wamefaulu kuua magaidi 22.
Afisa wa jeshi la Somalia, Farah Osman, ambaye alinukuliwa na shirika la habari la Reuters leo asubuhi amesema magari mawili yaliyokua yametegwa mabomu yalianza kulipukia magari ya tume ya Umoja wa Afrika na yale ya jeshi la Somalia.
Hata hivyo, shambulio hilo la jana dhidi ya kambi ya Bulomarer, kilomita 130 kusini magharibi mwa Mogadishu, liligharimu maisha ya askari kadhaa wa Amisom, kwa mujibu wa mashahidi.


AL SHABAB YAWASHAMBULIA AMISOM AL SHABAB YAWASHAMBULIA AMISOM Reviewed by safina radio on April 02, 2018 Rating: 5

No comments