CHOMBO CHA CHINA KILICHOPOTEA CHAINGIA KATIKA ANGA YA DUNIA LEO.
Chombo cha anga za
juu cha China kilichoharibika kimeingia katika anga la dunia asubuhi ya leo na
kupasuka vipande vipande kikitarajiwa kuanguka Kusini mwa Bahari ya Pasifiki.

Kituo cha anga za juu
cha China kimesema kupitia mtandao wake, kwamba chombo hicho, Tiangong-1,
kimeingia katika anga la dunia saa 2 na dakika 15 saa ya China, na kusisitiza
kuwa hakitasababisha uharibufu wowote.
Awali, wataalamu wa
masuala ya anga za juu walikuwa wamesema ingekuwa vigumu kujua chombo hicho
kingeanguka sehemu gani, hadi muda mfupi kabla ya kuingia katika anga la dunia.
Chombo cha Tiangong-1 kilipelekwa anga za juu
mwaka 2011, ikiwa hatua kubwa kwa China katika juhudi za kujenga kituo chake
binafsi cha anga za juu.
Mwaka 2016 chombo hicho kiliharibika, na
wanaanga wamekuwa wakisubiri kurejea kwake duniani. China imekanusha taarifa za
vituo vya anga vya kigeni, kwamba imepoteza udhibiti wa chombo hicho.
CHOMBO CHA CHINA KILICHOPOTEA CHAINGIA KATIKA ANGA YA DUNIA LEO.
Reviewed by safina radio
on
April 02, 2018
Rating:
No comments