WAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI UNAOTOLEWA NA WATAALAM
Wakulima hapa nchini wametakiwa kufuata ushauri
unaotolewa na wataalamu wa kilimo pale wanapoanza msimu wa kilimo ili waweze kujua njia bora za kuzalisha mazao
yao.
Ushauri huo umetolewa na Bi Edith Kadege mtaalamu wa
wadudu na magonjwa ya mazao kutoka kituo
cha utafiti wa kilimo Seliani Arusha wakati akizungumza na Redio Safina kuhusu
changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima hasa kipindi hiki cha msimu wa
kilimo.
Bi Kadege amesema kuwa wakulima wengi wanapoanza
kilimo chao wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea badala ya kuchukua maelezo
yanayotolewa na wataalamu wa kilimo hususani njia bora ya kuandaa mashamba yao
ambayo ndio njia mojawapo itakayomsaidia mkulima kupata mazao mengi.
Katika eneo la upatikanaji wa mbegu bora mtaalamu
huyo amesema kuwa kituo cha utafiti Seliani kimekuwa kikifanyia utafiti mbegu
mbalimbali ikiwemo Maharage na Mahindi kwa kuwa ndio mazao makuu yanayolimwa na
wananchi hivyo ni vyema wakulima wakafika katika kituo hicho pamoja na wakala
wa uuzaji wa mbegu ASA ili kupata mbegu hizo.
Hata hivyo
amewataka wakulima wanapokuwa na shida inayohusiana na kilimo kuwasiliana na
vituo vya utafiti vilivyoko katika maeneo yao ikiwemo cha kanda ya kaskazini
Seliani,Sua Morogoro na mkoani Tanga.
WAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI UNAOTOLEWA NA WATAALAM
Reviewed by safina radio
on
April 02, 2018
Rating:
No comments