DOLA ZAIDI YA MILIONI MBILI NA NUSU ZAIDHINISHWA NA SERIKALI YA KOREA KUSINI.


SEOUL

Taarifa ya Habari saa 01:00 mchana, 14 February, 2018.
Maafisa wa Korea kusini na Kaskazini wakikabidhiana makubaliano wa mashindano ya  Olympic ya majira ya bari mjini PyeongChang.

Maafisa wa Korea kusini wamesema serikali ya nchi hiyo iliidhinisha matumizi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni mbili na nusu kwa ushiriki wa Korea kaskazini katika michezo ya Olympic ya majira ya baridi iliyokuwa ikifanyika katika mji wa PyeongChang.

Fedha hizo zilitoka katika bajeti ya Ushirikiano wa Korea, italipia gharama zikiwemo za usafiri, malazi na chakula ya zaidi ya washiriki mia nne na washangiliaji wao.

Kamati ya kimataifa ya Olympic, itaangalia gharama za wanariadha wa Korea kusini.

Waziri wa Korea kusini Cho Myoung-gyon ameelezea ushiriki wa Korea kaskazini katika mashindano hayo kama tukio muhimu la kihistoria ambalo linafungua milango katika kupata amani katika Rasi ya Korea.

DOLA ZAIDI YA MILIONI MBILI NA NUSU ZAIDHINISHWA NA SERIKALI YA KOREA KUSINI. DOLA ZAIDI YA MILIONI MBILI NA NUSU ZAIDHINISHWA NA SERIKALI YA KOREA KUSINI. Reviewed by safina radio on February 14, 2018 Rating: 5

No comments