RAIS WA ZAMANI WA PERU ALBERTO FUJIMORI KUSHTAKIWA KWA MAUAJI
TAREHE 20-02-2018
Rais wa zamani wa
Peru ambaye alipewa msamaha hivi karibuni Alberto Fujimori, atashitakiwa kwa
mauaji ya mwaka 1992 ya wakulima sita, mahakama imetoa uamuzi huo siku ya
Jumatatu.
Uamuzi huo unakuja
wiki chache baada ya kiongozi huyo wa zamani, kupewa msamaha uliojaa utata na
kuachiwa kutoka kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa ya ukiukaji wa haki za
binadamu alioufanya kati ya mwaka 1999 na 2000 wakati akiwa madarakani.
Lakini mahakama siku
ya jumatatu ilitupilia mbali utetezi wake kwamba msamaha huo pia unajumuisha
kesi ya Pativilca, jina la wilaya ambako mauaji hayo yalitokea.
Wakosoaji wanasema
rais wa sasa Pedro Pablo Kuczynski ambaye alikuwa anakabiliwa na kura ya
kutokuwa na imani naye, alitoa msamaha kama malipo kwa mtoto wa Fujimori ambaye
ni mbunge na wenzake kutopiga kura ya kumuondoa madarakani.
RAIS WA ZAMANI WA PERU ALBERTO FUJIMORI KUSHTAKIWA KWA MAUAJI
Reviewed by safina radio
on
February 20, 2018
Rating:

No comments