KATIBU MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR DK.ABDUL HAMID MZEE AMESEMA VIONGOZI WA SERIKALI WANATAKIWA KUWA NA UWEZO WA KUJADILI MIKATABA
TAREHE 20-02-2018
Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dk. Abdul Hamid Mzee amesema viongozi wa serikali wanapaswa kuwa na
uwezo wa kujadili mikataba kabla ya kusaini ili kuondoa changamoto zinazoweza
kujitokeza.
Akizungumza Mjini Unguja wakati wa mafunzo ya siku
mbili ya kuwajengea uwezo Makatibu Wakuu na Manaibu wao kutoka wizara mbali
mbali za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Mzee amesema kuwa kosa dogo
linapotokea wakati wa kutia saini mikataba linaweza kulisababishia taifa
hasara.
Aidha, Dk. Mzee amesema kuwa kunakosekana utaalamu
unaohitajika wa kushughulika katika kusaini mikataba kutokana na kufanya kazi
kwa mazoea huku ulimwengu ukiwa
unabadilika na wenye wajanja wengi hivyo watendaji lazima wajengewe uwezo wa
namna ya kukabiliana na suala hilo hasa wanaposaini mikataba na makampuni
makubwa yenye uzoefu wa mda mrefu katika kazi.
Halikadhalika amebainisha kuhusiana na uwepo wa
uvumbuzi wa mafuta na gesi visiwani Zanzibar kutokana na Swala hilo kuwa jipya
na halijawahi kufanyika wisiwani humo ambapo watendaji wanaweza kukutana na
makampuni makubwa yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 50 katika kazi hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya
Uongozi inayoongoza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watedaji hao wa Zanzibar,
Kadari Singo amesema kuwa wanawajenga viongozi katika maeneo makuu watatu ambapo
kiongozi anapaswa kuwa na maamuzi ya kimkakati, kusimamia rasilimali za nchi
inavyopaswa, na kujijengea sifa binafsi za uongozi.
KATIBU MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR DK.ABDUL HAMID MZEE AMESEMA VIONGOZI WA SERIKALI WANATAKIWA KUWA NA UWEZO WA KUJADILI MIKATABA
Reviewed by safina radio
on
February 20, 2018
Rating:

No comments