SERIKALI YA MAGU YAIOMBA SERIKALI IWATATULIE KERO YA MAJI.


MWANZA.


Taarifa ya Habari saa 01:00 mchana, 14 February, 2018.
Bw. George Lutengano Mwalwiba, Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Magu.

Imeelezwa kuwa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza yenye wakazi zaidi ya laki tatu inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji hali ambayo imewafanya wananchi wake kuomba serikali iwatatulie kero hiyo.

Mkurugenzi wa Halimashauri ya Magu George Lutengano Mwalwiba amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa wanaendelea kutekeleza miridi mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji.

Naye, Kaimu Mhandisi wa maji Wilaya ya Magu Richard Mlilwa amesema kuwa changamoto hiyo imewalazimu kubuni miradi ya visima vya maji vinavyotumia nishati ya jua vinavyosaidia kutatua tatizo hilo la maji, kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa kamati ya maji toka moja ya vijiji vinne vyenye miradi hiyo.

Takwimu za upatikanaji wa maji katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza zinaonesha kwamba katika maeneo ya vijijini maji yanapatikana kwa asilimia 45 na eneo la mjini inapatikana kwa asilimia 20 pekee.

SERIKALI YA MAGU YAIOMBA SERIKALI IWATATULIE KERO YA MAJI. SERIKALI YA MAGU YAIOMBA SERIKALI IWATATULIE KERO YA MAJI. Reviewed by safina radio on February 14, 2018 Rating: 5

No comments