MAHAKAMA NCHINI KENYA YAAGIZA WAKILI MIGUNA KUREJESHWA NCHINI HUMO.
TAREHE 27-02-2018
Mahakama Kuu ya Kenya imeagiza mwanasiasa ambaye pia ni wakili wa upinzani Miguna Miguna aliyetimuliwa nchini humo mapema mwezi huu aruhusiwe kurejea nchini.
Bw Miguna alikamatwa na polisi kwa mchango wake katika kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa "rais wa wananchi", hafla iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru Park, mjini Nairobi mnamo mwezi Januari mwaka huu
Serikali ilikuwa imeeleza hatua hiyo ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa uhaini wa hali ya juu.
Bw Miguna, alikuwa mshauri wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipokuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ambapo Bw Miguna aliondolewa nchini humo na kupelekwa Canada baada ya kuzuiliwa kwa siku kadhaa.
Mahakama kuu imeamuru serikali kumpa Bw Miguna Miguna hati za kusafiria za kumuwezesha kurejea Kenya na kuhakikisha anasalia nchini humo hadi kesi yake dhidi ya serikali ikamilike kusikilizwa.
Kabla ya kuondolewa kwake nchini Kenya kwa nguvu mnamo Februari 7, serikali ilikuwa imekataa maagizo ya kumuwasilisha Bw Miguna mahakamani mara kadhaa.
Wakati wa kutimuliwa kwake, alipokonywa pasipoti yake ya Kenya hali iliyopunguza uwezekano wake wa kurejea Kenya kama raia wa wa nchi hiyo.

![]() |
WAKILI MIGUNA MIGUNA |

Reviewed by safina radio
on
February 27, 2018
Rating:

No comments