WAPIGANAJI WA KIKURDI NCHINI SYRIA WAMEWAKAMATA WANAMGAMBO WAWILI WA UINGEREZA WA KUNDI LA IS

TAREHE 09-02-2018

Image result for PICHA YA WAPIGANAJI WA SYRIA


Wapiganaji wa kikurdi nchini Syria wamewakamata wanamgambo wawili wa Uingereza wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS wanaojulikana kwa jukumu lao katika mateso na mauaji ya mateka wa nchi za magharibi.

Maafisa wa Marekani wamesema wapiganaji hao wawili wametambuliwa kuwa Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh ambao  walikuwa wanachama wawili wa mwisho wa kikundi kinachojiita Beatles cha wanamgambo wanne wa Uingereza waliokuwa mafichoni.

Habari zinaeleza kuwa Kiongozi wa wawili hao amejulikana kama Mohammed Emwazi, ambaye ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Kiarabu.

Jihadi John, kama alivyofahamika, alionekana akiwaua mateka, wakiwemo wanahabari wa Marekani Steven Sotloff na James Foley, ambapo video kadhaa za IS zilizoonesha watu wakikatwa vichwa.

 Habari za kukamatwa Kotey na Elsheikh ziliripotiwa kwanza na gazeti la New York Times, ambalo lilisema watu hao wawili wanazuiliwa na wanajeshi wa Kikurdi nchini Syria wanaoungwa mkono na Marekani katika ngome za mwisho za wanamgambo wa IS nchini Syria kwenye Mto wa Euphrates kusini mwa mpaka na Iraq.

WAPIGANAJI WA KIKURDI NCHINI SYRIA WAMEWAKAMATA WANAMGAMBO WAWILI WA UINGEREZA WA KUNDI LA IS WAPIGANAJI  WA KIKURDI NCHINI SYRIA WAMEWAKAMATA WANAMGAMBO WAWILI WA UINGEREZA WA KUNDI LA IS Reviewed by safina radio on February 09, 2018 Rating: 5

No comments