RAIS JACOB ZUMA AMEJIUZULU BAADA YA SHINIKIZO KUTOKA KWA CHAMA ANC.
![]() |
Mh. Jacob Zuma, Rais wa Afrika ya Kusini. |
Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtaka ampe nafasi makamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye kiongozi mpya wa chama hicho kwa sasa.
Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi.
Mapema Jumatano, polisi walivamia nyumba ya familia tajiri ya Gupta ambayo Zuma ana uhusiano wa karibu nayo ambapo baada ya Zuma kuwashukuru wale ambao amefanya nao kazi kwa miaka kadhaa huku akisema kuwa ghasia na migawanyiko ndani ya ANC imemsababisha ajiuzulu.
RAIS JACOB ZUMA AMEJIUZULU BAADA YA SHINIKIZO KUTOKA KWA CHAMA ANC.
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments