Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Suleman Jaffo amemwagiza Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Kisarawe kuandaa eneo maalum litakalotumika kujenga viwanda vidogo kuwezesha vijana hao kujiajiri.
PWANI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Suleman Jaffo amemwagiza Afisa Maendeleo ya
Vijana Wilaya ya Kisarawe kuandaa eneo maalum litakalotumika kujenga viwanda
vidogo kuwezesha vijana hao kujiajiri.
![]() |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Suleman Jaffo |
Waziri Jaffo ametoa agizo hilo Wilayani Kisarawe Mkoani
Pwani katika shughuli maalum ya kugawa vifaa vya ufundi kwa vikundi vya vijana kutoka
Kata za Kiluvya, Kurui na Marombo mkoni humo.
Aidha, Waziri Jaffo amesema kuwa suala la uatamizi
ni muhimu kwa vijana waliokwisha kujindeleza hivyo inapaswa waangaliwe kwa
karibu na uwezeshaji ili waendelee kuimarika katika shughuli zao kwa ajili ya
kuondoa suala la kuwapoteza vijana hao katika tasnia yao.
Pia, Waziri Jaffo ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya
hiyo kuvilea na kuviimarisha vikundi hivyo kimtaji kupitia asilimia tano za
mapato ya
ndani baada ya kunufaika na mradi wa kuwawezesha vijana kiuchumi wa YEE unaofadhiliwa
na umoja wa Ulaya na kusimamiwa na Plan Internatinal.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi VETA Dk. Bure Ngazi ameiomba jamii isiwafiche vijana wenye mahitaji
maalumu zinapotokea fursa za kuwawezesha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Suleman Jaffo amemwagiza Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Kisarawe kuandaa eneo maalum litakalotumika kujenga viwanda vidogo kuwezesha vijana hao kujiajiri.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments