KAMPUNI 37 ZASHINDA ZABUNI KWA KUSAINI MIKATABA 50 ZA UJENZI WA BARABARA, HALMASHAURI 9 MKOANI MTWARA.
MTWARA.
Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini-TARURA
mkoani Mtwara imesaini mikataba 50 na kampuni 37
zilizoshinda zabuni ya kujenga Barabara katika Halmashauri 9 mkoani humo.
Mratibu wa TARURA mkoa wa Mtwara
Mhandisi Seraji Mvuta
amesema miradi ya ujenzi wa barabara hizo zitakazogharimu fedha jumla ya shilingi
bilioni 4 unatarajiwa kukamilika
ndani ya mwaka huu wa fedha 2017/2018.
Aidha, Mhandisi Mvuta amesema kuwa
lengo la kutekeleza mradi huo katika kipindi cha mwaka huu wa fedha 2017/2018
ni kuhakikisha kuwa wanapanga kutekeleza miradi mingine katika mwaka wa fedha ujao.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoani humo Bw Elias Majisani amezitaka
kampuni zilizoshinda zabuni ya ujenzi wa barabara kutoa fursa za ajira kwa
wakazi wa maeneo husika wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ili nao waweze kunufaika.
Amesema kuwa hategemei kuona kuwa Mkandarasi anawachukua
vibarua katika mikoa ya Lindi au Mtwara mjini
kuwapeleka Tandahimba wakati kuna watu katika maeneo hayo wanaweza kufanya kazi za kawaida ambazo hazihitaji mtu kuwa na taaluma.
KAMPUNI 37 ZASHINDA ZABUNI KWA KUSAINI MIKATABA 50 ZA UJENZI WA BARABARA, HALMASHAURI 9 MKOANI MTWARA.
Reviewed by safina radio
on
February 16, 2018
Rating:

No comments