Naibu Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko amesema kuwa serikali inaendelea kuwawazesha wachimbaji wadogo wa madini vifaa kupitia ruzuku ya wachimbaji badala ya kutoa fedha taslim ambazo zimekuwa zikiombwa na wachibaji wasiokuwa na sifa.



KATAVI.

Naibu Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko amesema kuwa serikali inaendelea kuwawazesha wachimbaji wadogo wa madini vifaa kupitia ruzuku ya wachimbaji badala ya kutoa fedha taslim ambazo zimekuwa zikiombwa na wachibaji wasiokuwa na sifa.


Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara katika eneo la machimbo ya Kapanda Wilayani Mpanda  akiwa katika ziara ya siku moja ya kuangalia shughuli za wachimabaji katika mkoa wa  Katavi.

Aidha amebainisha kuwa fedha hizo za ruzuku zilizotolewa zinauwezekano wa kuwa zimetolewa kwa wachimbaji wasio wadogo bali kwa watu wachache wanaojua kuwasilisha masuala yao pamoja na kuwa na mtandao hadi ofisi za wizara.

Pia, amesema kuwa kuna viongozi ambao wanachukua fedha kutoka kwa watu hao takribani dola elfu hamsini hadi laki moja ambapo baada ya kupata fedha hizo walikwenda kufungulia biashara zao.

Hali kadhalika Mh. Biteko amesema kuwa kuna kiongozi ambaye amepatiwa fedha kiasi cha dola elfu hamsini sawa na shilingi milioni mia moja za Kitanzania na kuifanyia biashara kwa kununua ng’ombe na kusafirisha kwenda Dar es salaam kwa malori.

Awali akisoma risala,Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini kwa Mkoa wa Katavi Silibeti Sanga ameiomba serikali kuendelea kuwasaidia wachimbaji wadogo,kauli iliyoungwa mkono na Mwenyekiti wake Willium Mbogo.

Naibu Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko amesema kuwa serikali inaendelea kuwawazesha wachimbaji wadogo wa madini vifaa kupitia ruzuku ya wachimbaji badala ya kutoa fedha taslim ambazo zimekuwa zikiombwa na wachibaji wasiokuwa na sifa. Naibu Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko amesema kuwa serikali inaendelea kuwawazesha wachimbaji wadogo wa madini vifaa kupitia ruzuku ya wachimbaji badala ya kutoa fedha taslim ambazo zimekuwa zikiombwa na wachibaji wasiokuwa na sifa. Reviewed by safina radio on February 26, 2018 Rating: 5

No comments