RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.
![]() |
RAIS RAMAPHOSA |
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri, huku Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.
Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara ambapo Aliyekuwa mke wake Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais.
Bw Ramaphosa, ambaye ni mfanya biashara mwenye umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.
Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, akikataa shinikizo kubwa ya yeye kujiuzulu.
Utawala wa miaka tisa ya Bw Zuma ulikumbwa na misukosuko ya shutuma za ufisadi wakati nchi ilikuwa ikipambana na madeni ya ndani pamoja na viwango vya juu vya ukosaji ajira.
RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.
Reviewed by safina radio
on
February 27, 2018
Rating:
No comments