DK. SLAA NA MUHIDINI WAMEAPISHWA LEOKUWA MABALOZI WA SWEDEN NS NIGERIA. JIJINI DAR ES SALAAM.


DAR-ES-SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk John Magufuli leo amewaapisha Mabalozi wawili watakaowakilisha Tanzania katika nchi za Sweeden na Nigeria.



Hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam ambapo mabalozi walioapishwa ni pamoja na Dk. 
Wilbrod Peter Slaa ambaye anakuwa balozi wa Tanzania nchini   Sweeden na Muhidi Ally Muhoto anayekwenda nchini Nigeria.
Dk, Wilrod Peter Slaa.amekuwa Balozi wa Tanzania nchni Sweden. 

Bw. Muhidi Ally Muhoto amekuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa mabalozi hao naibu Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Suzan Alphonce Kolimba amesema wizara hiyo itahakikisha kuwa inatoa ushirikiano kwa mabalozi hao ili waende kuwakilisha vyema Tanzania katika nchi walizopangiwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Suzan Alphonce Kolimba akieleza jambo kwa mabalozi wapya.

Hata hivyo mara baada ya kuapishwa kwa mabalozi hao pia walikula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kinachotolewa na Kamishna wa Maadili hapa nchini Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela huku  mabalozi hao wakiahidi kutoa ushirikiano kwa serikali na kutekeleza viapo  vyao walivyoapa.

Mabalozi wapya wakila kiapo mbele ya rais wa Tanzania.






DK. SLAA NA MUHIDINI WAMEAPISHWA LEOKUWA MABALOZI WA SWEDEN NS NIGERIA. JIJINI DAR ES SALAAM. DK. SLAA NA MUHIDINI WAMEAPISHWA LEOKUWA MABALOZI WA  SWEDEN NS NIGERIA. JIJINI DAR ES SALAAM. Reviewed by safina radio on February 16, 2018 Rating: 5

No comments