LUTEN JENERALI YAKUBU HASSAN MOHAMED AAPISHWA KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA JWTZ.
DAR-ES-SALAAM.
Taarifa ya Habari 01:00 mchana, 15 February, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mh. Dk. John
Magufuli amemuapisha Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ.
Hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu jijini Dr es
salaam pia imetanguliwa kwa kupandishwa vyeo kwa takriban Mabrigedia Jenerali
kumi kutoka cheo cha Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali katika jeshi hilo.
Aidha, baada ya Rais Magufuli
kuridhia pendekezo la Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, JeneraliVenance Mabeho, amewapandisha vyeo, Meja Jenerali
Jacob Gidion Pingu kuwa katika kommandi NDC na Meja Jenerali Shilinyi Msungu kuwa Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa-JKT, kufuatia nafasi hizo kuwa wazi.
Vile vile, Jenerali Mabeho, ametaja
kuwapo kwa mabadiliko katika baadhi ya vitengo vya jeshi zikiwemo za Mkuu wa
Mafunzo Jeshini, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya vikosi chini
ya Makao Makuu ya Jeshi, huku akiwapandisha wakuu wa vitengo vya ukurugenzi, na
Msimamizi Mkuu wa Jeshi.
Kwa upande wake Waziri wa jeshi la ulinzi na
usalama nchini Hussen Ally Mwinyi, amepongeza kuapishwa kwa Luteni Jenerali
Yakubu Hassan Mohamed na kupandishwa vyeo kwa Mabrigedia Jenerali Kumi kuwa
Mameja Jenerali , huku akielezea sifa za Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ,kuwa
jeshi lenye linalofaa kuigwa katika bara la Afrika na Duniani kutokana na
nidhamu ya jeshi hilo.
Hata
hivyo Luteni Jenerali Yakubu Hassan
Mohamed amechukua nafasi hiyo
iliyokuwa inashikiliwa na Luteni Jenerali James Aloice Mwakibolwa baada
ya kustaafu kwake .
LUTEN JENERALI YAKUBU HASSAN MOHAMED AAPISHWA KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA JWTZ.
Reviewed by safina radio
on
February 15, 2018
Rating:

No comments