HALMASHAURIYA WILAYA YA SHINANGA IMEKAMILISHA JENGO LA WAGONJWA WA NJE YAANI OPD.
TAREHE 09-02-2018
Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga kupitia fedha za ruzuku kutoka serikali imekamilisha ujenzi
wa jengo la wagonjwa wa nje yaani OPD na nyumba moja ya watumishi pamoja na
jengo lakutolea huduma ya ushauri nasaha ambalo liko katika hatua za upauaji.
Hayo yamesemwa na
Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serkali za mitaa-TAMISEMI
Josephat Kandege wakati akijibu swali la Aza Hilal Hamad mbunge wa viti maalumu
aliyehoji kuwa serikali itapeleka lini fedha za kutosha kukamilisha ujenzi wa
hospitali ya wilaya ya shinyanga ambao umeamzishwa kwa nguvu za wananchi katika
mkutano wa kumi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea mjini
Dodoma.
Aidha, Mh. Kandege
amesema Jumla ya kiasi cha fedha shilingi milioni mia tatu sitini na tano zilitumika
kutoka katika vyanzo mbali mbali ambazo ni kiasi cha shilingi milioni mia mbili
sitini na saba ruzuku kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri ya
Wilaya shilingi milioni themanini na sita, nguvu za wananchi shilingi milioni
saba na mchango wa rais mstaafuu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete shilingi
miliolni tano.
Katika mwaka wa
fedha 2017/2018 zimetengwa silingi milioni mia moja na kumi kwa ajili ya
kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo ambapo kati ya fedha hizo shilingi
milioni arubaini ni mapato ya ndani ya halmashauri na shilingi milioni sabini
ni ruzuku kutoka serikali kuu.
Hali kadhalika kwa
mwaka wa fedha 2018/2019 zimetengwa shilingi milioni mia moja na kumi kwa ajili
ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo ambapo shilingi milioni hamsini ni
mapato ya ndani ya halamshauri ya wilaya na shilingi milioni sitini ni ruzuku
kutoka serikali kuu.
Hata hivyo serikali
itaendelea na ujenzi wa hospitali hiyo kulingana na upatikanaji wa fedha ili
wananchi waweze kupata huduma.
HALMASHAURIYA WILAYA YA SHINANGA IMEKAMILISHA JENGO LA WAGONJWA WA NJE YAANI OPD.
Reviewed by safina radio
on
February 09, 2018
Rating:
No comments