SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERKALI YA MAPINDIZI YA ZANZIBAR KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
sera,bunge,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Mh Antony Mavunde amesema kuwa
serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
MH.MAVUNDE |
Mh Mavunde ameyasema leo bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la mbunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar Mh Asha Abdalah
aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kupambana na wafanya biashara wa
madawa ya kulevya wanaotumia viwanja vya ndege vya Zanzibar kusafirisha madawa
hayo.
Amesema kuwa baada ya Tanzania bara kuanza kupambana
na watumiaji na wafanyabiashara hao kwa kuziba mianya ya kusafirisha madawa
hayo kupitia viwanja vyake vya ndege wafanyabiashara hao walihamia Zanzibar
hivyo ili kupambana na hali hiyo wameamua kushirikiana kupambana na wahusika
wote wanaohusika na biashara hiyo haramu.
Katika hatua nyingine naibu waziri Mavunde amesema
kuwa serikali ina mpango wa kuanzisha madirisha ya kuwahudumia waathirika wa
matumizi ya madawa ya kulevya katika hospitali za mikoa lengo likiwa ni
kuwasaidia kuwapa matibabu waathirika hao kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo bunge la 11 mkutano wa 11 umenza leo
bungeni mjini Dodoma mkutano ambao utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kujadili na
kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.
SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERKALI YA MAPINDIZI YA ZANZIBAR KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments