ISRAEL YAFIKIA MAKUBALIANO NA UMOJA MATAIFA.


Serikali ya Israel imesema imefikia makubaliano na Umoja wa Mataifa ya kuwapeleka katika nchi za Magharibi kiasi ya Waafrika elfu kumi na sita wanaoomba hifadhi.

Image result for picha ya waziri mkuu wa israel benjamin netanyahu
NETANYAHU

Mpango huo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR, utafanikisha kuwapeleka kiasi ya wahamiaji zaidi ya elfu 16 kati ya elfu thelathini na saba kwenye nchi za Ujerumani, Canada na Italia.

Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa Israel wameupinga mpango huo, wakisema kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, hakuwaarifu kabla kuhusu makubaliano hayo.

Ujerumani na Italia pia zimeelezea wasiwasi wao kuhusu mpango huo baada ya kila mmoja kusema hawakufahamishwa kuhusu hilo.

Ofisi ya Netanyahu imesema mpango huo utachukua nafasi ya mpango uliowekwa awali wa kuwarejesha wahamiaji kwenye nchi ya Afrika ambayo ilikuwa haijatajwa.

ISRAEL YAFIKIA MAKUBALIANO NA UMOJA MATAIFA. ISRAEL YAFIKIA MAKUBALIANO NA UMOJA MATAIFA. Reviewed by safina radio on April 03, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.