SHIRIKA LA ECHO KUENDELEA KUPIGA VITA GUGU KAROTI
Shirika la lisilokuwa la kiserikali la ECHO
linalofanya kazi na wakulima na wafugaji limefanikiwa kutoa elimu ya kuthibiti
gugu karoti kwa shule za msingi na sekondari za jiji la Arusha kwa lengo la
kuwaepusha na madhara yatokanayo na majani hayo.
PICHA YA GUGU KAROTI |
Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa
Shirika la ECHO nchini Malvery Begry, wakati akizungumza na waandishi wa habari
jinsi ambavyo wamekuwa wakielimisha jamii na shule mbali mbali namna ya kudhibiti
jani hilo.
Bw. Begry, amesema kuwa kutokana na majani hayo aina
ya gugu karoti kuwa na madhara kwa wakulima na wafugaji na hata wanafunzi
mashuleni wameweza kutoa elimu kuhusiana na jani hilo ili waweze kuepuka athari
za majani hayo.
Aidha, amesema kuwa mbali na kutoa elimu hiyo
wamekuwa wakishirikiana kwa pamoja na viongozi wa vijiji kung’oa majani hayo
ambayo yamekuwa yakiathiri afya za wananchi pamoja na mifugo.
Kwa upande wake Bw Shamba wa Shirika hilo Charles
Bonivencha amesema kuwa kutokana na majani hayo kuwa na madhara ya kiafya kwa
binadamu wamekuwa wakihamasisha jamii kuhakikisha wanang’oa majani hayo na
kuyachoma ili waweze kulitokomeza.
SHIRIKA LA ECHO KUENDELEA KUPIGA VITA GUGU KAROTI
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments