SERIKALI YA LIBYA YAANZA OPERESHENI YA MASHAMBULIO DHIDI YA DAESH.
Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imetangaza kuwa jeshi lake
limeanza kutekeleza operesheni ya mashambulio dhidi ya kundi la kigaidi la
DAESH magharibi mwa nchi hiyo.
Kupitia taarifa iliyotoa hapo jana, serikali ya umoja wa kitaifa
ya Libya imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limeanza kutekeleza operesheni ya
kijeshi ya kuwasaka wanachama wa Daesh ambao wangali wanaendesha harakati zao magharibi
mwa nchi.
Muhammad As-Salik,ambaye ni msemaji wa Waziri Mkuu wa serikali
ya umoja wa kitaifa ya Libya Fayez al-Sarraj amesema, miongoni mwa malengo
ya operesheni hiyo ya kijeshi ni kuvilenga vituo na ngome zote za kigaidi
kandokando ya mji wa Misrata ulioko kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu
Tripoli.
Libya imekuwa ikishuhudia ongezeko la harakati za makundi ya
kigaidi, na hali ya mchafuko pamoja na
matatizo ya kisiasa na kiuchumi tangu yalipojiri mabadiliko ya kisiasa mwaka
2011 na kuvurugika uthabiti uliosababishwa na uingiliaji kijeshi wa Marekani na
shirika la kijeshi la NATO.
SERIKALI YA LIBYA YAANZA OPERESHENI YA MASHAMBULIO DHIDI YA DAESH.
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments