MAFURIKO YAWAACHA WATU BILA MAKAZI NA KUHARIBU EKARI 50 ZA MAZAO YA CHAKULA, ARUSHA.
Zaidi ya
kaya kumi (10) zimeachwa
bila makazi kufuatia mafuriko ya
mvua zilizonyesha usiku wa
kuamkia leo katika
kata ya Bwawani wilayani
Arumeru mkoani Arusha ikiwa ni
pamoja na uharibifu
wa takribani ekari 50 za
mazao ya chakula.
Wananchi waachwa bila makazi kutokana na mafuriko. |
Akizungumzia
maafa hayo ndugu Jeremia Kisiongo mollel mwenyekiti wa
kitongoji cha darajani kijiji cha
kigongoni amesema kuwa mazao ya chakula
yaliyoharibiwa na mvua ni mahindi pamoja na maharage sambamba na miundombinu ya barabara.
Aidha wakati
akiambatana na Msafara wa wasamaria wema mwenyekiti huyo
umeshuhudia baadhi ya
familia zikilazimika kuhamisha
familia zao kwenda
kuwatafutia hifadhi kwa ndugu
na jamaa walioko kata za
jirani huku wengine
wakiwa wanatumia ndoo , plastiki na
sufuria kusomba maji yaliyojaa
ndani ya nyumba
zao huku mifugo ikikosa hifadhi.
Kufuatia hali
hiyo Bw kisiongo ametumia
fursa hiyo kuomba msaada kwa
wasamaria wema,serikali ya wilaya pamoja na mkoa
wa Arusha kutembelea eneo hilo ili
kujionea kiwango cha madhara yaliyosababishwa na mvua hizo na kuwasaidia wahanga wa mvua hizo
kusudi wasipatwe na madhara yatokanayo
na mafuriko ya
mvua.
Akizungumza na
redio safina mmoja kati wanaharakati wafuatiliaji kiwango
cha uharibifu wa
mvua katika maeneo hayo
ndugu Frenki Lobulu
Mollel amesema kuwa leo majira ya
jioni baadhi ya familia
zilizokosa makazi ni pamoja
na nyumba za boma
la Kiroroma na
nyumba za Boma
la Namoyo katika
eneo la kitongojini katika kata hiyo .
MAFURIKO YAWAACHA WATU BILA MAKAZI NA KUHARIBU EKARI 50 ZA MAZAO YA CHAKULA, ARUSHA.
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments