Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamesema huenda umoja huo ukaiwekea Cam bodia vikwazo ikiwa nchi hiyo haitasitisha hujuma dhidi ya demokrasia na utawala wa kisheria.
BRUSSELS.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamesema
huenda umoja huo ukaiwekea Cam bodia vikwazo ikiwa nchi hiyo haitasitisha
hujuma dhidi ya demokrasia na utawala wa kisheria.
![]() |
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini (Kushoto) akisalimiana na waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Uhispania, Jose Manuel Garcia-Margallo mjini Brussels |
Mawaziri hao wameonya kuhusu hali ya kutisha ya
kudorora kwa demokrasia, heshima kwa haki za binadamu na utawala wa sheria
pamoja na kuongezeka kwa ukandamizaji wa wapinzani, vyombo vya habari na
wanaharakati nchini Cam bodia.
Mawaziri hao wameihimiza nchi hiyo kurejesha
demokrasia na wameitaka serikali kuwashirikisha viongozi waliochaguliwa katika
mazungumzo muhimu, baada ya chama kikuu cha upinzani kuvunjwa kwa lazima mwezi
Novemba mwaka uliopita.
Umoja wa
Ulaya pia umeelezea wasiwasi wake kwa hatua ya kukamatwa kwa kiongozi wa
upinzani wa Cam bodia Kem Sokha, na imeishauri Cam bodia kukoma kutumia
mahakama kama kifaa cha kisiasa kuwahangaisha wanasiasa wa upinzani na
wanaharakati wengine.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamesema huenda umoja huo ukaiwekea Cam bodia vikwazo ikiwa nchi hiyo haitasitisha hujuma dhidi ya demokrasia na utawala wa kisheria.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments