WAZIRI LUKUVI AMEZITAKA HALMASHAURI ZOTE KUKAMILISHA ZOEZI LZA UKUSANYAJI KODI YA ARDHI IFIKAPO APRILI 30 MWAKA HUU
TAREHE 20-02-2018
Halmashauri
za wilaya na
manispaa kote nchini zimetakiwa kukamilisha
zoezi la ukusanyaji
kodi ya ardhi
kwa asilimia miamoja
hadi ifikapo aprili
30 mwaka huu kabla
ya serikali kuzichukulia
hatua halmashauri zitakazoshindwa kutekeleza
agizo hilo .
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa ardhi na maendeleo ya nyumba na
makazi Mh. Wiliam
Lukuvi katika
kikao cha watendaji
wa idara ya
ardhi wilayani Bukoba
mkoani Kagera alipokuwa
katika ziara yake
ya kikazi mkoani
humo.
Mh,Lukuvi amelazimika kutoa kauli
hiyo kufuatia kusikitishwa
kwake na hali
ya ukusanyaji wa
kodi kwa baadhi
ya idara za
ardhi hapa nchini
ikiwemo wilaya Bukoba
ambayo kwa mwaka
wa fedha wa
serikali 2017/2018 Imeshindwa
kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi
ya ardhi kwa
asilimia mia moja kama ilivyojipangia
Amesema kuwa Halmashauri ya
wilaya ya Bukoba
ilikusanya kodi ya
shilingi milioni 100 kati
ya milioni 500
zilizopaswa kukusanywa 2017/2018
makusanyo ambayo Mh,waziri
aliyaona ni hafifu
kulingana na malengo
yaliyowekwa .
Hata
hivyo imebainika kuwepo
kwa baadhi ya
halmashauri ambazo
zimewamilikishia watu ardhi
kwa kuwarasimisha huku
ardhi zenyewe zikiwa
hazijapimwa kisheria hali
ambayo huisabishia serikali hasara
ama kutoa mwanya
kwa wanyonge kuonewa
na baadhi ya watu
wenye dhamana na matajiri
WAZIRI LUKUVI AMEZITAKA HALMASHAURI ZOTE KUKAMILISHA ZOEZI LZA UKUSANYAJI KODI YA ARDHI IFIKAPO APRILI 30 MWAKA HUU
Reviewed by safina radio
on
February 20, 2018
Rating:

No comments