ZAIDI YA SHILINGI BILIONI BILIONI ZATOLEWA KWA UJENZI WA MAEGESHO YA KIVUKO CHA LINDI-KITUNDA.


LINDI.

Serikali imetoa zaidi  shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maegesho ya Kivuko cha Lindi-Kitunda ili kuwawezesha wananchi wa Kitunda kutekeleza shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi mkubwa.

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa wakati akikagua ujenzi wa mradi huo katika ziara yake ya siku moja mkoani Lindi.

Amesema kuwa wanachi wa eneo hilo walikuwa wanachangamoto nyingi hasa kipindi bahari ikichafuka ambapo walikuwa wakipata ugumu katika kusafiri kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Pia, ameongeza kuwa upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kwa wananchi ulikuwa ukipatikana kwa ugumu hasa huduma za afya kutokana na kutokuwapo kwa mawasiliano rafiki ya usafiri ya moja kwa moja kutoka Kitunda kwenda Lindi kwa kuwa hudumu nyingi zinapatikana Lindi.

Hali kadhalika, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imelitambua suala hilo na iliahidi kujenga maegesho ya kivuko pamoja na kuleta kivuko ambapo ujenzi wa kivuko umekamilika kwa asilimia tisini na tisa na itakamilika mwishoni mwa wiki hii ili kukabidhiwa na Mkandarasi wa mradi huo.

Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa maegesho hayo hatua itakayofuata ni kuletwa kwa kivuko hicho kitakachotumika kuimarisha mawasiliano kati ya Kitunda na Lindi.




ZAIDI YA SHILINGI BILIONI BILIONI ZATOLEWA KWA UJENZI WA MAEGESHO YA KIVUKO CHA LINDI-KITUNDA. ZAIDI YA SHILINGI BILIONI BILIONI ZATOLEWA KWA UJENZI WA MAEGESHO YA KIVUKO CHA LINDI-KITUNDA. Reviewed by safina radio on March 06, 2018 Rating: 5

No comments